單集摘要
Msikilizaji, je, wajua kuwa gazeti la zamani linaweza kugeuzwa kuwa penseli na wakati huo huo kutoa ajira kwa vijana? Huo ndio ubunifu wa wajasiriamali wawili katika eneo la Athi River nchini Kenya ambao wamegeuza magazeti yaliyotumika kuwa fursa ya biashara na chanzo cha kujikimu kimaisha.
Msikilizaji, je, wajua kuwa gazeti la zamani linaweza kugeuzwa kuwa penseli na wakati huo huo kutoa ajira kwa vijana? Huo ndio ubunifu wa wajasiriamali wawili katika eneo la Athi River nchini Kenya ambao wamegeuza magazeti yaliyotumika kuwa fursa ya biashara na chanzo cha kujikimu kimaisha.
單集
Gazeti linapogeuzwa kuwa penseli ya kuandikia
已收聽Msikilizaji, je, wajua kuwa gazeti la zamani linaweza kugeuzwa kuwa penseli na wakati huo huo kutoa ajira kwa vijana? Huo ndio ubunifu wa wajasiriamali wawili katika eneo la Athi River nchini Kenya ambao wamegeuza magazeti yaliyotumika kuwa fursa ya biashara na chanzo cha kujikimu kimaisha.
DRC: Ufugaji wa nyuki unavyokwamua maisha ya raia wa mji wa Goma
已收聽Mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, unaendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama na kiuchumi, huku ukiwa chini ya udhibiti wa waasi wa FRN wanaoongozwa na rais wa zamani Josephu Kabila, ambako fursa za ajira ni chache na vijana wengi wanakabiliwa na changamoto ya kujipatia kipato, hata hivyo baadhi yao wameamua kutafuta njia mbadala za kujikimu na kusaidia familia zao.
Afrika kuzindua taasisi ya ukadiriaji mikopo, je itasaidia?
已收聽Afrika imezindua rasmi Wakala wa Ukadiriaji wa Mikopo wa Afrika, Africa Credit Rating Agency (AfCRA), hatua inayolenga kushughulikia changamoto za gharama kubwa za mikopo na kuvutia uwekezaji zaidi kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo. Je, kuanzishwa kwake kutapunguza kweli gharama za mikopo kwa mataifa ya Afrika, au ni mwanzo tu wa safari ndefu ya mageuzi ya kifedha?
Je, Afrika itapata sauti inayodai katika uchumi wa dunia?
已收聽Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni na gharama za juu za kukopa katika masoko ya kimataifa. Fedha nyingi ambazo zingetumika katika afya, elimu, miundombinu na ajira zinaishia katika kuhudumia madeni, hali inayoweka shinikizo zaidi kwa uchumi wa nchi hizi. Je, hitaji la Afrika la kuwa na mfumo mpya wa kifedha duniani wenye uwakilishi na usawa zaidi litawezekana?
Kiwanda cha kusafisha mafuta Lamu: mwanzo wa mapinduzi ya nishati Afrika Mashariki?
已收聽Kenya inaagiza karibu mahitaji yake yote ya bidhaa za Petroli kutoka nje, hii ikiwa na maana kuwa bei na upatikanaji wa mafuta katika nchi hii, na kwa kiasi kikubwa katika ukanda unaweza kuathiriwa na mambo yanayotokea katika masoko ya kimataifa, hata hivyo habari njema ni kuwa bilionea wa Afrika Aliko Dangote anajenga kiwanda cha kusafisha mafuta huko Lamu. Kwanini hatua hii ni muhimu? Tufuatilie